Aliyewahi kuwa Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, amefariki dunia leo tarehe 11 Desemba 2025 jijini Dodoma.

Taarifa ya msiba huu imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.

Mussa Azzan Zungu, kupitia Kitengo cha Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge. Akitoa taarifa hiyo, Spika Zungu alisema: "Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo jijini Dodoma."

Aidha aliwapa pole Waheshimiwa Wabunge, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho kutokana na msiba huo mzito.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaendelea kuratibu mipango ya mazishi, na taarifa zaidi zitatolewa kadri taratibu zitakavyokamilika.

Marehemu Mhagama aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, zikiwemo nafasi kadhaa za uwaziri.

Mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) katika Serikali ya Rais John Magufuli, kabla ya kuhamishiwa Ofisi ya Rais kushughulikia tawala Bora mwaka 2022.

Alichukuliwa kama kada madhubuti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja wa wabunge waliodumu kwa muda mrefu, akihudumu kama Mbunge wa Peramiho kwa miaka mingi