Marekani imeitoa dhamana za usalama kwa Ukraine kwa kipindi cha miaka 15, amesema Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, wakati wa mazungumzo kuhusu mpango wa amani uliorekebishwa na Donald Trump huko Florida Jumapili.
Rais wa Marekani alisema kwamba makubaliano kuhusu suala hili yamekaribia kufikiwa kwa "asilimia 95%", lakini kiongozi wa Ukraine amesisitiza kwamba angependa dhamana hizo ziwe hadi miaka 50.
Rais Zelensky alieleza masuala ya eneo na kiwanda cha nyuklia kilichotawaliwa na Urusi huko Zaporizhzhia kama mambo ya mwisho yanayohitaji suluhu, na hatma ya eneo la Donbas lililo na utata nchini Ukraine.
Urusi awali ilikataa sehemu muhimu za mpango huo, lakini msemaji wa Kremlini alikubaliana Jumatatu na tathmini ya Trump kwamba amani iko karibu, ripoti ya shirika la habari la Urusi Tass iliripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya mkutano wa Jumapili, Zelensky alirudia imani yake kwamba makubaliano ya amani kwa jumla yamefika 90%, ni takwimu aliyotoa kabla ya ziara hiyo.
Viongozi wa Marekani na Ukraine pia walionyesha kwamba kumekuwa na maendeleo kuhusu kizuizi kimoja muhimu, dhamana za usalama kwa Ukraine. Shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba Zelensky anatumai dhamana yoyote ya usalama itaanza mara Kyiv itakaposaini makubaliano ya amani.
"Pasipo dhamana za usalama, vita hivi haviwezi kuonekana vimeisha kweli. Hatuwezi kukiri kwamba vimeisha, kwa sababu tukikabiliwa na jirani kama huyu bado kuna hatari ya shambulio jipya," Zelensky alieleza, kulingana na ripoti ya AFP.
Aliongeza kwamba anataka Marekani "kuzingatia zaidi uwezekano wa miaka 30, 40, 50".
Marekani bado hajajibu kuhusu kuongezwa kwa muda huo. Jumapili, Trump alisema makubaliano yako karibu kufikiwa.

0 Comments