Staa wa kitambo wa muziki wa dansi au rhumba Bongo, Christian Bella hatimaye amepewa uraia wa Tanzania baada ya kuishi na kufanya muziki nchini kwa takribani miaka 20.
Uraia wa Bella ambaye anajulikana kimuziki kama King of the Best Melodies umetangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene leo Alhamisi, Desemba 18, 2025 ikiwa ni Siku ya Wahamiaji duniani ambapo Waziri Simbachawene amesema Tanzania kuna idadi kubwa ya wahamiaji na baadhi yao wamekuwa wakipewa uraia.
Katika harakati zake za muziki hapa nchini, Bella alijiunga na bendi ya Akudo Impact, ambapo alitoa wimbo wake wa kwanza Walimwengu si Binadamu. Alianza safari yake ya muziki akiwa na kundi la vijana wenye vipaji, akiwemo Fally Ipupa, ambaye baadaye alijiunga na Koffi Olomide.
Akiwa na umri wa miaka 16, Bella alijaribu kujiunga na bendi ya Koffi Olomide lakini hakupata nafasi ya kutumbuiza jukwaani, hali iliyomfanya ajiunge na Akudo Impact.
Hata hivyo, alikusudia kurejea kwa Koffi baada ya muda. Kabla ya kufanya uamuzi huo, alishauriwa kutoa wimbo mwingine wa Kiswahili baada ya Walimwengu si Binadamu, na hivyo akaachia kibao “Yako Wapi Mapenzi,” ambacho kilipata umaarufu Kabla ya kupewa uraia wa Tanzania, Bella alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

0 Comments