Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Tuggar ameomba msamaha Burkina Faso kufuatia tukio ambapo ndege ya kijeshi ya Nigeria iliingia bila kibali katika anga ya Burkina Faso na kusababisha wanajeshi 11 wa Nigeria kuzuiliwa.
Msemaji wa Tuggar aliiambia BBC kwamba maafisa waliozuiliwa wameachiwa na walipaswa kurejea Nigeria, bila kusema ni lini.
Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kuelekea Ureno ilipopata tatizo la kiufundi na kulazimika kutua Burkina Faso, kwa mujibu wa Jeshi la Wanahewa la Nigeria.
Hatua hiyo iliibua mzozo wa kidiplomasia na Muungano wa Nchi za Sahel (AES) unaojumuisha Burkina Faso na majirani zake, Mali, na Niger.

0 Comments