DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteua  Plasdus Mbossa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, imesema: “Plasdus Mkeli Mbossa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)”.