
DAR ES SALAAM: SERIKALI imeombwa kupunguzu ushuru wa kodi za magari nchini ili kuwapa Watanzania wenye vipato vya kati na chini nafasi ya kununua magari na kurahisisha shughuli zao.
Khatibu Hussien, Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya magari ya Harmony Auto ya nchini China ametoa ombi hilo leo wakati wa uzinduzi wa duka la maonyesho ya magari aina ya BYD Shark 6 jijini Dar es Salaam.

Amesema ushuru unapokua mkubwa na bei ya magari inakuwa juu pia, hivyo hatua ya kupunguza ushuru itafanya Watanzania wengi kupata nafasi ya kuwa na magari.
Akizungumzia ubora magari hayo, Khatibu Hussein amesema yana teknolojia ya kisasa ya umeme na mafuta ( plug-in hybrid) inayoruhusu betri kujijaza chaji yenyewe hata inapokuwa imeisha mafuta.

“Hili gari linaweza kutembea kwa umeme kwa zaidi ya kilomita 100 baada ya kuchajiwa kwa saa 2 tu,” amesema Khatibu Hussien.
Amesema teknolojia hiyo inategemea kuwasili Tanzania hivi. karibuni huku hatua za kufikisha teknolojia hiyo ikiwa inaendelea.

Duka hilo la maonyesho ya magari lipo Barabara ya Nyerere jirani na uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
MENEJA wa Tawi BYD Tanzania, Lee Ming ameeleza kuwa upanuzi wa kampuni hiyo ni mkakati wa kukuza nishati jadififu na kutoa suluhisho bora utanzaji mazingira Afrika.

Amesema kwa sasa kampuni hiyo inafanya kazi Afrika Kusini, Tanzania, Kenya na Msumbiji.

Amesema kuwa magari yanayopatikana Tanzania kwa sasa yana mifumo ua uendeshaji kwa lugha ya Kiingereza hata hivyo kwa lugha ya Kiswahili mkakati unaandaliwa.
0 Comments