Muwanga Kivumbi anatuhumiwa kuandaa mashambulizi kwenye vituo vya polisi – jambo ambalo chama chake kinakanusha
Polisi nchini Uganda wamemkamata mbunge na mshirika wa karibu wa kiongozi wa upinzani Bobi Wine kwa madai ya kuhusika katika ghasia zilizohusiana na uchaguzi wiki iliyopita.
Muwanga Kivumbi, naibu kiongozi wa Wine's National Unity Platform (NUP), anatuhumiwa kuandaa mashambulizi kwenye kituo cha polisi na kituo cha kujumlisha kura baada ya kushindwa kwao katika uchaguzi, jambo ambalo chama kinakanusha.
Polisi wamesema kuwa watu saba waliuawa katika tukio hilo, lakini mwanasiasa huyo ametoa maelezo tofauti, akisema kuwa watu 10 waliuawa nyumbani kwake wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa ubunge.
Jeshi la Polisi la Uganda lilisema katika chapisho la X siku ya Alhamisi kwamba Kivumbi "atafikishwa mbele ya mahakama kwa wakati ufaao".
"Kukamatwa kwake kunahusiana na matukio ya hivi majuzi ya vurugu za kisiasa," iliongeza.
Kukamatwa kwa Kivumbi kunafuatia mvutano baada ya uchaguzi wa wiki jana ambapo Rais Yoweri Museveni alichaguliwa tena kwa muhula wa saba.

0 Comments