Rais wa Bunge la Ulaya amesema, "Kuanzia mitaa ya Tehran hadi katikati mwa Bunge la Ulaya, ujumbe uko wazi: Iran lazima iwe huru, Iran itakuwa huru."
Roberta Metsola aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba Bunge la Ulaya "lilipiga kura kwa wingi mno kuunga mkono matarajio ya watu wa Iran."
Aliandika kwamba Bunge la Ulaya limeitaka serikali ya Iran kuchukua hatua madhubuti "kukomesha ghasia" na kukomesha "ukandamizaji wa kikatili na mauaji makubwa ya waandamanaji wa amani."
Kwa mujibu wa Bi Metsola, Bunge la Ulaya pia limetoa wito wa "kusitishwa kwa hukumu ya kifo" na kuiambia Iran kwamba ni lazima "ikomesha mara moja mauaji ya serikali yanayotekelezwa ili kunyamazisha upinzani."
Kwa mujibu wa Rais wa Bunge la Ulaya, wanachama wa taasisi hii wanatoa wito wa kuachiliwa kwa wale waliowekwa kizuizini na "waandamanaji wote waliowekwa kizuizini na wafungwa wa kisiasa."
Taasisi hiyo muhimu ya Ulaya pia imetoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya vipengele vya ukandamizaji nchini Iran, "Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu litangazwe kuwa shirika la kigaidi" na maafisa wake kufunguliwa mashtaka.
Mwishoni mwa ujumbe huu, Bibi Metsola pia aliwaandikia watu wa Iran: “Hata nyaya zikikatwa tunasikia sauti yako, hata kukatika kwa umeme tunakuona, hauko peke yako. Bunge la Ulaya linasimama nawe kidete.

0 Comments