
KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amemuagiza msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Puge kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika ifikapo Machi 10, 2026.
Kihongosi ametoa maagizo hayo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na kupokea taarifa kuwa mradi huo umechelewa kukamilika. Awali, ujenzi huo ulitarajiwa kukamilika Oktoba 2025, lakini haujakamilika kutokana na kuchelewa kwa utolewaji wa fedha kupitia mifumo ya malipo ya mradi wa Barrick.
Shule hiyo, ambayo imepandishwa hadhi na kuwa ya kidato cha tano na sita, inajengwa kupitia ufadhili wa mradi wa Barrick kwa gharama ya Sh milioni 450. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mabweni mawili, vyumba sita vya madarasa pamoja na matundu 10 ya vyoo. Kwa sasa, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,004 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tano. SOMA: Kihongosi aagiza anayedaiwa kumtorosha mwanafunzi asakwe
0 Comments