Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, Aprili 15, 2026 imetengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo itatolewa baadaye Saa 9:00 Alasiri.

0 Comments