Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa China imekubali “kutotuma silaha za kijeshi nchini Iran” baada ya kumuandikia rais wa China Xi Jinping, na kumtaka asifanye hivyo.
Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema “China imefurahi kuwa tutafungua mlango bahari wa Hormuz, nafanya kwa ajili yao na pia dunia”
“Hali hii haitawahi kurudia tena, wamekubali hawatatuma silaha Iran,” Aliandika Trump.
“Tunafanya kazi pamoja kwa busara, si hiyo inashinda kupigana? Kumbuka tuko vizuri kwa kupigana ikiwa itatubidi, vizuri kushinda kila mtu”
Siku ya Jumanne, China ilisema hatua ya Trump kufunga mlango bahari wa Hormuz “ni kutowajibika” na ni kudhoofisha makubaliano ya kusitisha mapigano.
China pia ilipinga taarifa kuwa walikuwa wanapanga kutuma silaha nchini Iran.

0 Comments