Waziri mkuu wa Uingereza, Keir Starmer amesema hatashinikizwa kuliingiza taifa lake katika vita vinavyoendelea Iran.
Kiongozi huyo amesema hivyo baada ya Rais Trump kusema hapo jana katika mahojiano kuwa makubaliano ya kibiashara kati ya Marekani na Uingereza yanaweza kutupilia mbali wakati wowote.
Akizungumza akiwa bungeni, Starmer aliwaambia wabunge kuwa “hivi si vita vyetu, tumekuwa tukipokea shinikizo nyingi ili tubadilishe msimamo wetu”
“Sitabadilisha mawazo yangu, hatuna maslahi kama taifa kwa vita hivyo”

0 Comments