Baada ya tukio la risasi lililotokea mjini Washington, viongozi mbalimbali wa dunia wametoa ujumbe wa pole, mshikamano na kulaani tukio hilo linaloonekana la kisiasa, huku wakieleza furaha yao kwamba Rais Donald Trump na waliokuwepo walinusurika na wako salama.

Mark Carney – Waziri Mkuu wa Canada

Anasema amefarijika kwamba Rais Trump, mke wake, na waliokuwepo wote wako salama. Anaongeza kuwa mawazo yake yako kwa wote waliotikiswa na tukio hilo la kushtua.

Anthony Albanese – Waziri Mkuu wa Australia

Anasema amefurahi kusikia kuwa wote waliokuwepo eneo la tukio wako salama. Pia anapongeza kazi ya vyombo vya usalama kwa hatua za haraka.

Kaja Kallas – Mwakilishi - Umoja wa Ulaya

Anaonyesha uungaji mkono wake kwa Rais Trump, mkewe na wageni wote, akisisitiza kuwa vurugu za kisiasa hazina nafasi katika demokrasia.

Delcy Rodríguez – Rais wa mpito wa Venezuela

Analaani vikali kile alichokiita shambulio lililoshindwa, na anawatakia kila la heri wote waliokuwepo kwenye tukio hilo.

Shehbaz Sharif – Waziri Mkuu wa Pakistan

Anasema ameshtushwa sana na tukio hilo, na anatuma maombi yake kwa Rais Trump na wote walioathirika na tukio hilo.

Narendra Modi – Waziri Mkuu wa India

Anatuma salamu za heri na kuwatakia usalama na afya njema Rais, mkewe na Makamu wa Rais.

Claudia Sheinbaum – Rais wa Mexico

Anasema “tunatoa heshima zetu,” akisisitiza kuwa vurugu hazipaswi kuwa njia ya kutatua tofauti katika jamii yoyote.