KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiroameweka wazi kuwa vurugu zilizotokea Oktoba 29 mwaka 2025 zimetia doa katika taifa la Tanzania lakini limeweza kuvuka kipindi kile na kubaki kuwa Taifa moja.


Dk.Migiro ameyasema hayo alipokuwa ajibu maswali ya mtangazaji wa Crown Media Salim Kikeke aliyekuwa akifanya mahojiano maalumu na Katibu Mkuu huyo kuhusu hali ambayo Taifa limepitia baada ya vurugu za Oktoba29.

Katika swali lake Kikeke alisema kuna watu kutoka vyama vya vingine na wengine kutoka ndani ya CCM wanazungumza mambo ambayo ukiyatazama unaona kimsingi kama yanaligawa Taifa badala ya kulileta pamoja, hivyo akataka kujua msimamo wa Chama Cha Mapinduzi katika hilo

“Pamoja na kwamba wapo wanaopaza sauti hizo lakini ukweli ni tumebaki kuwataifa moja, tumeendeelea kuendesha shughuli zetu za kiuchumi na kijamii bila kutetereka ndani muda mfupi,amani ilirejea,uchumi wetu bado umebaki tulivu na tunajua duniani kuna vyombo vya kupima,kutathimini ukuaji wa uchumi.

Vyombo vyote vimeeleza hata baada ya kadhia ile ya Oktoba 29 uchumi wetu umebaki tulivu.

“Hii inaonesha sio tu ustahimilivu ,inaonesha tumeendeelea kuwa taifa moja tukiwa na njia moja ya kujijenga kijamii na kiuchumi lakini utaona hali hii ya umoja na utulivu haipimwi tu na sisi wa ndani au Chama Cha Mapinduzi .Tumeona baada ya  tukio lile bado watu wameendelea kuwa na imani na taifa hili, wameendeelea kuona utulivu wetu umerejea.”

Akiendelea kujibu Dk.Migiro amesema Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi aliwapokea wawekezaji kutoka mataifa matano.Pia taifa limepokea wafanyabiashara kutoka Urusi huku akiongeza China pia imeendelea kuwekeza.

“Na siku za karibuni Mwakillishi Mkazi wa Kanda hii wa Benki ya Dunia alikwenda kumuaga Rais wetu baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi katika kanda hii na alimueleza kuwa Tanzania bado ina maoteo mazuri ya kukua kwa uchumi.

“Kwahiyo siamini kama tungekuwa ni taifa lililogawanyika haya yote yangetokea nawapo tumewasikia wanaosema taifa limegawanyika ,limepasuka.Chochote wanachokiona ambacho ni kiashiria cha kugawanyika au kiashiria cha mpasuko Mtanzania yeyote ambaye ana mapenzi mema na taifa letu atakuwa na sauti ya kuunganisha ,sio sauti ya kuleta mpasuko na hili linakuwa na umuhimu zaidi kwa watu kama sisi viongozi .

“Nimewahi kuwa kiongozi kwa nafasi yangu ndogo mpaka ngazi ya Uwaziri. Kitaifa nimepata heshima kubwa ya kufanya kazi nyingine katika taifa letu ,nilikuwa mpaka Julai mwaka jana nilipata heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kitalaam ya uandishi wa Dira ya Taifa 2050 .Niheshima kubwa na ni sehemu ya uongozi ambao nilipata heshima ya kuwa nayo.

“Kwa maana hiyo ninapozungumza lazima kauli yangu iakisi dhamana na heshima niliyopewa ya kuwa kiongozi .Sauti yangu kama kiongozi au viongozi wengine wawe wa kijamii , dini au kisiasa. Kiongozi wa kweli ni yule anayepaza sauti ya kukubali kuna kitu kilitupata lakini kusema kwamba tusiendelee kukaa kwenye kadhia hii kwa namna ya kuendeleza mpasuko,”amesema Dk.Migiro na kusisitiza hakuna mgawanyiko.

Pia amesema viongozi wanawajibu wakuhakikisha wanaendelea kwa kauli zetu navitendo vyao kushikamana kama taifa nakuimarisha umoja wetu .

Kuhusu ripoti ya Jaji Chande kuwa walibaini uwepo wa picha za akili unde ambazo zilitizamwa na kuna madai pengine kuna picha zinasingiziwa akili unde ili kuficha yaliyotokea Oktoba 29 na nini maoni yaCCM

Dk.Migiro amejibu kuna picha ambazo akiliunde lakini kuna picha ambazo ni za matukio ya zamani zimeunganishwa na matukio ya Oktoba 29 na tume imeeleza ziko picha ambazo ni za matukio yasehemu nyingine nje ya nchi lakini zimeunganishwa.

“Sasa tume ilipokuwa inaeleza metholodojia iliyotumia ilisema \wametumia watalaam wautambuzi kutambua zile picha ni za lini ,zawapi na za wakati gani. Hayo ni masuala yakitalaam .Mimi na wewe ndugu Kikeke sidhani kama tuna nafasi kubwa yakuzungumzia utalaam wa aina hii.

“Wewe mwenzangu ni mtalaam wa mambo ya habari kama hivi unavyonihoji .Mimi ninataaluma yangu ndogo ya sheria lakini sikusomea sheria ya utambuzi .Nadhani itakuwa vema na busara tukawaachia watalaam wakachambua hili na tunaamini baada ya Tume ya Upelelezi wa Jinai kumaliza kazi yake tutapata mwanga zaidi kuonesha mambo zaidi yalikuaje Oktoba 29 na baadae nini kilitokea,”amesemaDk.Migiro.