
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameshiriki mdahalo maalum wa uzinduzi wa taarifa ya African Economic Outlook 2026 ambapo ametoa taswira ya jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na mageuzi katika sekta ya fedha.
Akizungumza katika mdahalo huo jana jioni (Jumanne, Mei 26, 2026) katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kintele (Kintele International Conference Centre), jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, Waziri Mkuu alisema Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta binafsi na kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani katika kuimarisha uhamasishaji wa rasilimali za ndani.

“Hatua hizo zinaenda sambamba na uamuzi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuunda tume ya kupitia mifumo ya kodi, usimamizi wa kodi, pamoja na viwango vya kodi, kwa lengo la kufanya mfumo wa ukusanyaji kuwa rafiki zaidi na kuongeza wigo wa mapato ya Serikali.”
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la mwezeshaji wa mdahalo huo, Dkt. Joy Kategekwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uratibu na Ushirikiano wa Kikanda wa Benki ya AfDB ambaye alimtaka Waziri Mkuu aeleze uzoefu wa Tanzania katika usimamizi wa fedha za umma na jinsi ambavyo imefanikiwa kufikia bajeti ya nchi inatumia asimilia 70 ya mapato ya ndani.

Akitoa ufafanuzi zaidi, Dkt. Mwigulu alisema Tanzania iliamua kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kuiongezea ufanisi Mamlaka ya Mapato ikiwemo kuweka mifumo ya ukusanyaji kwa kutumia njia za kidijitali kama vile mashine za EFD na kufanya malipo kwa njia za mitandao ya simu.
“Mamlaka za Serikali za Mitaa ziliimarishwa kwa kuruhusiwa kukusanya mapato yasiyo ya kikodi na tukahakikisha kuwa kunakuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kila senti inayokusanywa (prudency) na wananchi waliona fedha zao zinatumika katika miradi hiyo,” alisema na kuongeza:

0 Comments