Dakika 90 na zile 30 za nyongeza za mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Arsenal na PSG zilikamilika huku timu zote mbili zikiwa sare ya 1-1. Mikwaju ya penati ikaamua mshindi PSG ikipata penati 4- 3.
Arsenal walitangulia kwa bao la mapema lililofungwa na Kai Havertz katika dakika ya 6, kabla ya PSG kusawazisha kupitia penalti ya Ousmane Dembélé katika dakika ya 65.
Mchezo umekuwa na ushindani mkali, Arsenal wakionekana kuwa na nidhamu nzuri ya ulinzi huku PSG wakitawala zaidi umiliki wa mpira na kujaribu kutengeneza nafasi.
PSG inakuwa timu ya pili kuandika historia katika muongo uliopita kwa kuweza kutetea taji hilo, ililolitwaa msimu uliopita kwa kuchapa Inter Milan 5-0, ikifuata nyayo za Real Madrid
0 Comments