
Kati ya bajeti hiyo, Sh bilioni 39 zimetengwa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa wizara, Sh bilioni 28 kwa ajili ya matumizi mengineyo ya uendeshaji, huku Sh bilioni 458.1 zikielekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ametoa ombi hilo wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Mei 04, bungeni jijini Dodoma.
0 Comments