Donald Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Marekani inaendelea kufanya mazungumzo na Iran lakini amesisitiza kuwa usitishaji wa mapigano umefutiliwa mbali.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuomba kuendelea na mazungumzo. Tumekubali ombi hilo, lakini Marekani imewaeleza wazi kwamba usitishaji wa mapigano umefutwa."

Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika majimbo matano kusini mwa Iran, kufuatia mashambulizi dhidi ya meli zilizokuwa zikipita eneo hilo.

Marekani na Iran zimetupiana lawama kwa kushindwa kudumisha makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa.

Aidha, maafisa wa Iran wamesema nchi hiyo ina haki ya kujibu mashambulizi yoyote yanayolenga miundombinu yake.