Gazeti la Marekani, Wall Street Journal, limeandika kuhusu makubaliano ya ulinzi ya Makkah yaliyosainiwa na Saudi Arabia, Uturuki na Pakistan, likisema makubaliano hayo yanaashiria mabadiliko katika mwelekeo wa ushirikiano wa kikanda wa Saudi Arabia.
Gazeti hilo limesema muungano mpya unaibuka Mashariki ya Kati, ambao unaweza kuitwa “Mikataba ya Makkah”.
Hata hivyo, limesema muungano huo si ule wa Saudi Arabia, Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Marekani ilikuwa ikitarajia, bali ni makubaliano ya pamoja ya ulinzi yaliyosainiwa Ijumaa katika mji mtakatifu wa Makkah.
Chini ya makubaliano hayo, nchi hizo tatu zenye Waislamu wengi wa Sunni zimekubaliana kuwa shambulizi la kijeshi dhidi ya nchi moja litachukuliwa kuwa shambulizi dhidi ya nchi zote.
Wall Street Journal pia imeeleza wasiwasi kuhusu ushiriki wa Uturuki na Pakistan, ikisema nchi hizo zinaonekana kuwa na misimamo yenye utata katika masuala ya kupambana na ugaidi.
Gazeti hilo limemkosoa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa kumkaribisha na kumuunga mkono Hamas, huku likisema uhusiano wa Pakistan na Taliban pamoja na al Qaeda ni tata.
0 Comments