Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote amezindua uuzaji mkubwa wa hisa kuwahi kufanyika barani Afrika, kupitia mauzo ya hisa ya IPO katika kiwanda chake cha kusafisha mafuta.
Dangote ambaye ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika, anauza takriban asilimia tatu ya hisa za kiwanda hicho katika mpango aliouita “IPO ya wananchi”. Tajiri huyo amesema lengo lake ni kuwapa raia wa kawaida wa Nigeria fursa ya kuwa sehemu ya mafanikio ya kiwanda hicho.
Kiwanda hicho kimenufaika kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kusafisha mafuta na bidhaa zingine kutokana na vita vinavyoshuhudiwa mashariki ya kati haswa nchini Iran.
Dangote amesema lengo la uuzaji huo wa hisa ni “kuwezesha wananchi wa kawaidia kushiriki katika kutengeneza utajiri.”
0 Comments