Mwanadada muigizaji Judith.

Muigizaji Judith amewapa mashabiki wake jambo jipya la kuzungumza baada ya kuonyesha gari lake jipya, huku akifichua kuwa gari hilo limemgharimu Sh milioni 160 na kwamba hakulinunua kwa kudunduliza fedha.

Judith ametoa ufafanuzi huo baada ya kuwapo kwa taarifa zilizokuwa zikidai kuwa gari hilo lina thamani ya Sh milioni 90. Muigizaji huyo amekanusha taarifa hizo na kusema yeye alilinunua kwa Sh milioni 160, huku akisisitiza kuwa alilipa fedha hizo taslimu.

Judith amesema mafanikio hayo ni sehemu ya matokeo ya kazi yake, akieleza kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii usiku na mchana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Judith aliweka picha za gari hilo na kuandika ujumbe huu:

“Baraka zinazovaliwa kwa uzuri. 🥷
Gari hili ni kwa ajili ya wanawake warembo pekee. 😎

Sura mpya. Moyo uleule.
Bado najifunza, bado nakua na bado nimeweka miguu yangu chini.

Kumbuka: Aina hii ya gari ni kwa ajili ya wanawake warembo tu, na si kwa wanaume 😂

Uzuri, kujiamini na kusudi — taji limevalishwa. 👑✨
Hongera kwa malkia wote wa Miss Grand! ”

Baada ya ujumbe huo, mashabiki walijitokeza kwa wingi kumpongeza Judith, huku baadhi yao wakimtania kuwa gari hilo ni mwanzo wa kupata magari makubwa zaidi.

Nana Dollz alimpongeza huku akisema: “Range Rover mwakani , mambo mengi mazuri zaidi yanakuja .”

Shabiki mwingine alitania kuhusu kauli yake ya kwamba gari hilo si la wanaume, akisema: “Naondoka na sentensi ya mwisho  ‘si kwa wanaume’. Hongera babe .”

Wengine waliendelea kumpongeza kwa ujumbe mbalimbali kama “Hongera tajiri,” “Msichana wangu,” “Hongera mama,” huku wakitumia emoji za moto na moyo kuonyesha furaha yao.

Wakati huohuo, Judith amekuwa akitajwa kwenye mitandao kufuatia tetesi za kuachana na mpenzi wake ambaye awali alikuwa akihusishwa naye.

Baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa uhusiano huo umefikia mwisho, ingawa madai hayo bado ni tetesi.

Pamoja na gumzo hilo, Judith kwa sasa ameendelea kuonyesha mafanikio yake, huku gari hilo jipya likiwa miongoni mwa vitu vilivyoibua gumzo kubwa kwa mashabiki wake.