Mazishi ya watoto 27 waliofariki katika mkasa wa moto shuleni yanafanyika mjini Bukavu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Tayari majeneza 27 yamewasili katika Shule ya Ibanda. Watoto hao walifariki katika moto uliotokea wiki iliyopita katika shule za Furaha na Ujamaa.

Familia za waathiriwa na maafisa wamekusanyika kwa ibada kabla ya mazishi kufanyika katika Makaburi ya Ruzizi.

Katika Shule ya Ibanda, iliyoko kando ya Ziwa Kivu, bango kubwa limewekwa kuomboleza waathiriwa wa moto huo.

Waasi wa M23, wanaodhibiti eneo la Bukavu, wamesema watoto wengi waliuawa katika msongamano wakati wakijaribu kutoroka kutoka madarasani ila bado kisa cha moto huo haujabainika.

Serikali ya Kinshasa, kwa upande wake, imetoa wito wa uchunguzi huru kufanyika ili kubaini chanzo cha moto huo na waliohusika. Waathiriwa kadhaa walionusurika bado wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Viongozi wa M23, Corneille Nangaa na Bertrand Bisimwa, wamehudhuria mazishi hayo