Salamu za rambirambi zinaendelea kumiminika kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa michezo wa Afrika Kusini, Owen Ndlovu, ambaye alipatikana amefariki dunia saa chache baada ya kutekwa nyara wakati wa tukio la uporaji wa gari karibu na Johannesburg.
Kwa mujibu wa polisi, Ndlovu, mtangazaji wa zamani wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC), alitekwa Jumanne alipokuwa akimchukua mkewe kutoka kanisani katika eneo la Katlehong.
Mwili wake ulipatikana na wakazi asubuhi ya Jumatano, huku mashuhuda wakisema ulikuwa na majeraha ya risasi.
Polisi wameanzisha msako wa watu watatu wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo na wanaendelea kuchunguza mazingira ya mauaji hayo.
Kisa hicho kwa mara nyingine kimeibua mjadala kuhusu viwango vya juu vya uhalifu wa vurugu vinavyoendelea kuikabili Afrika Kusini.
0 Comments