Viongozi, wageni mbalimbali, viongozi wa dini, wasanii na watu kutoka kada tofauti wamefika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Rais Samia amewasili nyumbani kwake Kizimkazi leo, Septemba 8, 2026, baada ya mumewe kufariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Miongoni mwa waliomtembelea Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye alifika kutoa pole kufuatia msiba huo.

Viongozi wa dini pia wameungana na waombolezaji kumfariji Rais Samia, akiwemo Mtume Boniface Mwamposa pamoja na Mchungaji Tony Kapola.

Aidha, wasanii mbalimbali wamefika Kizimkazi kutoa pole na kumfariji Rais Samia katika kipindi hiki cha majonzi.

Msiba huo umeendelea kuwakutanisha viongozi na wageni mbalimbali wanaofika Kizimkazi kutoa pole kwa Rais Samia na familia ya Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.