
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Humphrey Elisamon, maarufu kama Msoka, mwenye umri wa miaka 63, mkazi wa eneo la Mtaa wa Mungu Mwema, Hongoro, Kibamba, jijini Dar es Salaam, anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa panga kichwani na Dickson Elimringi Msoka, mwenye umri wa miaka 22, ambaye ni mtoto wake wa kambo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam Oktoba 19, 2026, tukio hilo limetokea Oktoba 18, 2026, ambapo mtuhumiwa alishambuliwa na wananchi kabla ya Jeshi la Polisi kufika eneo la tukio.Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa katika hali mbaya baada ya kushambuliwa na wananchi, na baadaye alipoteza maisha akiwa anapelekwa hospitalini.
Uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.
Jeshi la Polisi Dar es Salaam limetoa wito kwa wananchi kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kijamii, wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa, viongozi wa dini na wadau wengine, katika kutatua changamoto za kijamii, kiuchumi, kisheria na kidini, ili kuepusha matukio yanayoweza kusababisha madhara makubwa.

0 Comments