Mahakama ya Usuluhishi wa migogoro ya Michezo (CAS) imeahidi kutoa uamuzi haraka kuhusu rufaa ya Senegal baada ya kunyang'anywa taji la soka la Kombe la Mataifa ya Afrika kutokana na wachezaji wao kutohudhuria mechi ya mwisho, ambalo lilitolewa kwa mwenyeji wa Morocco. Mahakama ya juu zaidi ya michezo ilisikiliza hoja Alhamisi na inatarajiwa kutoa uamuzi wake "ndani ya siku chache."
Hoja hiyo ilisikilizwa kwa zaidi ya saa tano nyuma ya milango iliyofungwa.
Vikao hivyo vilifanyika katika jiji la Lausanne nchini Uswizi, yapata miezi kumi baada ya Pape Gueye kufunga bao la ushindi kwa Senegal katika muda wa ziada dhidi ya wenyeji, kufuatia muda wa kawaida kuisha kwa utata.
"Najua umekuwa ni muda mrefu waa kusubiri kwa mashabiki, miezi kadhaa baada ya fainali kati ya Senegal na Morocco," alisema Matthieu Reeb, Mkurugenzi Mkuu wa Mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.
Aliongeza kuwa "Ratiba na taratibu za kesi ziliwekwa kwa makubaliano na pande zinazohusika katika kesi hii. Kwa hivyo kila mtu alikuwa akijua ratiba, na lengo letu kama Mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo, kama mamlaka kuu, ni kutoa uamuzi haraka iwezekanavyo baada ya kusikilizwa kwa kesi... (Alhamisi)."

0 Comments