Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatafanya shambulio dhidi ya Iran kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula uliopangwa kufanyika Novemba 3, akibainisha kuwa Washington inafanya mazungumzo "yenye tija" na Tehran, huku utawala wake ukitangaza vikwazo vipya kwenye sekta ya mafuta ya Iran.
Matamshi ya Trump siku ya Alhamisi yalikuja baada ya bei ya mafuta kupanda kutokana na ripoti za vyombo vya habari zilizozungumzia uwezekano wa mashambulizi mapya ya Marekani dhidi ya Iran kabla ya uchaguzi, huku kukiwa na mvutano wa kijeshi unaoendelea katika eneo hilo.
Trump aliandika kwenye jukwaa lake la Truth media: "Nataka kuweka wazi kwa kila mtu kwamba licha ya hali mbaya sana ambayo Iran iinakabiliana nayo, kiuchumi na kijeshi, hatutaishambulia Iran wakati wowote kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula."
Aliongeza kuwa: "Tuna mazungumzo yenye matunda na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," bila kutoa maelezo zaidi.
Matamshi haya ya Trump yanakuja wakati ambapo juhudi zinaendelea kukomesha vita vilivyozuka Februari iliyopita, kufuatia mashambulizi yaliyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.

0 Comments