Nchi mbalimbali pamoja na Umoja wa Mataifa zimelaani shambulizi la waasi wa Houthi nchini Yemen katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh, Saudi Arabia, lililosababisha vifo vya watu wasiopungua 12 na kujeruhi zaidi ya 300.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amelitaja shambulizi hilo kuwa baya sana, akisema nchi yake inatathmini uwezekano wa kujiunga na Saudi Arabia katika operesheni za kijeshi dhidi ya waasi hao. Trump pia amesema anatarajia kuzungumza na kiongozi mkuu wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelilaani shambulizi hilo na kusema mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia yanakiuka sheria za kimataifa na yanapaswa kusitishwa mara moja.
Nchi nyingine zilizolaani shambulizi hilo ni pamoja na Misri, Qatar, Pakistan, Jordan, Oman, Palestina na Syria, huku zikionya kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu muhimu yanatishia amani na usalama wa eneo hilo.
Ni shambulio la tatu kufanywa katika Uwanja huo ndani ya wiki moja.

0 Comments