Akifunga kambi hiyo Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Malawi, Bw. Bestone Chisamile. amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa inatekeleza kwa vitendo ushirikiano wa matibabu ya kibingwa 

"Ushirikiano wa Afya kati ya Malawi na Tanzania unatekelezwa kupitia kambi ya matibabu ya kibingwa nchini Malawi. Hata hivyo tumeanza Majadiliano, yataangazia manufaa ya kambi hiyo kwa wagonjwa pamoja na umuhimu wa kurasimisha ushirikiano mpana zaidi unaojumuisha huduma za matibabu, mafunzo ya wataalamu, masuala ya dawa na rufaa za wagonjwa." amesema Bw. Chisamile

Timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania imefanya upasuaji kwa wagonjwa 64 haya yote yamewezekana chini ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali za nchi hizi mbili.

"Madaktari na wataalamu kutoka Tanzania walileta ujuzi na uzoefu katika fani mbalimbali za matibabu na kubadilishana maarifa na wenzao wa Malawi, pale Mzuzu katika hospitali ya Mzuzu na hapa Lilongwe katika Hospitali Kamuzu" Bw. Chisamile

Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Agnes Kayola amesema hii imekuwa ni fursa kubwa kwa wanchi wa malawi na madaktari

"Kambi hii imewanufaisha wagonjwa zaidi ya 810,katika hao 64 wamefanyiwa upasuaji 49 wamepewa rufaa ya kwennda Hospitali ya Benjamin Mkapa faida nyingine ya kambi hii imewezesha pia kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma kati ya wataalamu wa afya wa nchi hizi mbili." Amesema Balozi Kayola

Kambi hii ilianza tarehe 28/09/2026 na imehitimishwa leo ikiwa ni ushirikiano wa BMH,SOTAC na MSD, kambi hii inamagari ya kisasa yenye chumba chaupasuaji inayowezesha kutoa matibabu katika mazingira yoyote.