Rais wa Marekani Donald Trump amesema watu wanaovujisha taarifa kuhusu operesheni za kijeshi za nchi hiyo kwa vyombo vya habari “wanapaswa kupigwa risasi”.
“Nadhani wanaovujisha taarifa wanapaswa kupigwa risasi,”
alisema Trump katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bullhead City, Arizona, Jumatano. “Zamani, tulikuwa tukiwapiga risasi watu waliovujisha taarifa kama vile taarifa za nchi iliyokuwa inakwenda kushambuliwa.”Akizungumzia shambulio la Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwezi Juni 2025, Trump alidai kuwa mtu fulani alikuwa amefichua muda wa kuondoka na kuwasili kwa ndege za kijeshi za Marekani zilizotumika kutekeleza operesheni hiyo.
Donald Trump alikosoa kuchapishwa kwa taarifa hizo katika vyombo vya habari, vikiwemo magazeti ya New York Times na kituo cha televisheni cha CNN. Alisema watu waliohusika na uvujishaji huo wanapaswa kupewa adhabu kali, akiwataja kuwa “watu waovu zaidi duniani.”

0 Comments