Vikosi vya Yemen vimetangaza kuwa vinaendesha mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran katika mji mkuu, Sana'a, na eneo la Saada, ambalo limekuwa ngome kuu ya kundi hilo.

Msemaji wa kijeshi alisema vikosi vyao vilikuwa vikishambulia maeneo ambayo aliyataja kuwa muhimu sana.

Hata hivyo, mwandishi wa BBC alisema kuwa inaonekana Saudi Arabia pia ilishambuliwa, baada ya moshi na miale ya moto kuonekana ikipanda kutoka katika kituo cha mafuta cha kampuni ya Aramco.

Tangu kuanza kwa vita na Iran, kundi la Houthi limetangaza kuzuia usafirishaji wa majini kuelekea Saudi Arabia, huku likishambulia maeneo muhimu na meli, na kutwaa maeneo ya kimkakati katika pwani ya Bahari ya Shamu.