
DAR ES SALAAM: Dar sasa ni full shangwe! Staa wa Nigeria Young Jonn ametua rasmi Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea 4Plays, sherehe za miaka minne za 1245.
Hitmaker huyo anatarajiwa kupanda jukwaani Superdome Arena, Masaki, Oktoba 17, kwenye usiku unaokuja na mchanganyiko wa muziki, nightlife na full Mega club experience energy.
Young Jonn ataungana na Marioo pamoja na wasanii wengine kuhakikisha anniversary hii inaacha historia mjini.
Shughuli hii imedhaminiwa na Don Julio, Heineken, Clouds Media, Johari Rotana na Air Tanzania.
John Saviours Udomboso, anayejulikana katika tasnia ya muziki kama Young Jonn, ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki kutoka Nigeria, ambaye kwa sasa amesajiliwa chini ya lebo ya muziki ya Chocolate City Music.
Mwimbaji huyo pia anajulikana kwa nyimbo zake maarufu za Dada na toleo lake la remix aliloshirikiana na Davido.
0 Comments