Vikwazo zaidi vya kiuchumi na kisiasa vinazidi kutolewa dhidi ya Laurent Gbagbo, Rais wa Ivory Coast ambaye amekataa kuondoka madarakani baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baraza kuu la umoja wa mataifa sasa limemtambua rasmi mpinzani wa bwana Gbagbo, Alassane Ouattara, kuwa ndiye rais wa haki wa taifa la Ivory Coast.