Ukweli ukichukua nafasi uongo hukosa nafasi,Bidada Mariam toka Bongo Star Seach akieleza hisia zake jinsi yaliyomkuta kati Hotel waliyokuwa wamepangiwa washiriki wa kumtafuta huyoo mmoja wa wenye kipaji cha juu katika fani ya kuimba.akieleza bila aibu alinena hayaa.. "Kiukweli toka nizaliwe sikuwahi kuona kitu Jacuzzi au bomba la maji ya mvua,kitu ambacho kiliniwia vigumu sana jinsi gani ya kutumia vifaa hivyo pale nilivyokutana navyo hotelini humo kwani binafsi sikuzaliwa katika mazingira hayo akinena bidada" Mariam.
Kusikia hivyo, Maza House alitabasamu kisha akamwambia asihofu, kwani hakuna kiumbe anayeweza kufahamu mambo yote na ndivyo ilivyokuwa kwake kuhusiana na bafu la mvua!