Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo mh. Emmanuel Nchimbi akihutubia ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambapo katika sehemu ya hotuba yake amewataka vijana kujiandaa kikamilifu kwa majukumu yaliyo mbele yao kwani Idara nyingi za serikali na Mashirika binafsi viongozi na watendaji ni vijana.