Ni kitu cha kawaida kabisaa kwa wenzetu kushangaa...kwa tamaduni au desturi zetu huwa tunamshangaa sana mtu anayeshangaa na kumuona kana kwamba ni mshamba kumbe sisi kwa kushangaa kule tunaonekana washamba.Pichani ni baadhi ya matajiri wakubwa nchini Abu Dhabi wakilishangaa kombe linaloshindaniwa nchini Uingereza kwenye English Premier League.Wananchi wa huko ameliomba rasmi liende kule ili watu wakalione na kujifunza baadhi ya mambo kutokana na kombe hilo.
Watoto nao ambao hawakuwa nyuma katika kueleweshwa zaidi juu ya kombe hilo ambalo watu wengi duniani wanavutiwa na Ligi ya hukoo Uingereza kwa kuangalia kupitia kwenye maluninga yao.Watu wengi walijitokeza kulishangaa kombe hilo ambalo kwa macho linavutia zaidi kuliko kuliona kwenye picha.
Mtoto mdogo akijibiwa maswali yake anayouliza kutokana na kile anachokiona kimeandikwa kwenye mabango kama ujioneavyo.Mabango hayo yameandikwa baadhi ya kumbukumbu za wachezaji na matukio mabalimbali kuhusiana na ligi kuu ya Uingereza.
Unachotakiwa hapo ili kuliona Kombe hilo ni kufuata taratibu ambazo zimewekwa uwanjani hapo.pichani baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni ili kufuata taratibu zote nao wapate kuliona kombe hilo.kwa wenzetu ukishangaa watakushangaa.