MASTAA wanaotesa katika anga la muziki Bongo, Maunda Zorro, Abubakar Kisongo ‘Mandela’ na Hussein Rashid ‘Machozi’ wameonekana kukatika mishipa ya aibu na kufanya mambo ya chumbani sehemu zisozofaa, Risasi Mchanganyiko limewanasa na ushahidi mzito mkononi.

Kamera ya gazeti hili ikiwa kazini wikiendi iliyopita katika mitaa mbalimbali ya jijini Dar es Salaam, ilifanikiwa kuwafuma wasanii hao wakifanya mambo ya kimahaba katika sehemu mbalimbali na nyakati tofauti.

MANDELA
Mnenguaji wa kiume ‘front line’ wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Abubakar Kisongo ‘Mandela’ alikuwa wa kwanza kunaswa usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita, mishele ya saa 10 na dakika zake alfajiri akiwa nyuma ya Ukumbi wa Masai Club, Kinondoni, Dar.

Mandela alikuwa ‘busy’ akifanya mchezo mchafu na msichana anayejulikana kwa jina la Jacky Michael, ‘chapchap’ paparazi wetu akafyatua picha za kutosha na kuhifadhi kwenye makabrasha yetu (angalia yenye afadhali ukurasa wa nyuma).



Mandela alipomuona mwandishi wetu aliishia kumchimba mkwara kwa kumwambia: “Oya acha ujinga bwana, watu tusifurahie mambo yetu kisa nyie? Sasa ole wako hizo picha nizione gazetini, utanitambua mimi ni nani. Mnashindwa kufanya mambo ya msingi mnaanza kufuatilia maisha ya wenzenu.”

HUSSEIN MACHOZI
Pamoja na kufahamika kwa upole wake, msanii wa Bongo Fleva, Hussein Rashid ‘Machozi’ alifanya tukio la aibu lililotengeneza kichwa cha habari hii, Jumapili usiku katika chobingo moja baada ya kumaliza kupiga shoo katika ukumbi mmoja wa burudani uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Awali alikuwa akidendeka na msichana huyo, lakini alipomuona paparazi wetu alibadilisha mkao, alipoulizwa kulikoni wanaonekana katika mahaba mazito kiasi hicho, alisema eti hakuna chochote zaidi ya kupozi na shabiki wake (angalia picha).
“Huyu ni shabiki wangu tu, hapa anaonesha ni jinsi gani ananikubali. Hakuna kibaya chochote kaka, ujue mimi nina mchumba wangu hivyo siwezi kumsaliti hata kidogo,” alisema Machozi.

MAUNDA ZORRO
Mkali wa Bongo Fleva, Maunda Zorro naye ameingia kwenye listi hii baada ya ‘kukamatwa’ katika ukumbi aliokuwa msanii mwingine wa tasnia hiyo Hussein Machozi.Maunda alikuwa amejiachia na mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina lake, njemba hiyo ilimbambia sawasawa huku ikimwangushia mabusu kila baada ya muda, hivyo kuzua hisia za mapenzi kati yao kwa watu waliokuwa wakiwatazama.

Maunda alipopewa nafasi ya ‘kujitetea’ alijibu kwa kifupi: “Bwana hapa tupo kwenye starehe zetu, sasa maswali baadaye na huyu ni jamaa yangu.”