Kizuizi cha kimataifa kwa Zimbabwe kuuza almasi zake kutoka kwenye machimbo ya mashariki ya Marange kimeondolewa na chombo kinaratibu madini hayo.

Baraza la Almasi Duniani (WDC) limesema linakaribisha uamuzi huo uliofikiwa baada ya mazungumzo yaliyohusisha Marekani, Muungano wa Ulaya na nchi za Afrika.

Muungano wa Ulaya na Marekani zilizuia juhudi za awali za kuondoa marufuku hiyo.

Ilipitishwa mwaka 2009 kufuatia tuhuma kuwa maafisa wa jeshi la Zimbabwe kuwa na mkono katika madini hayo.

Mkuu wa sera za nje wa Ulaya Catherine Ashton amesema Muungano wa Ulaya umeondoa marufuku hiyo kwa sababu "kuwajibika upya kwa Zimbabwe kushughulikia eneo hilo kutokana na ukiukwaji wa haki", Shirika la Habari la Reuters linaripoti.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano nchini DRC na chombo kinachosimamia na kutoa kibali cha biashara ya almasi Kimataifa Kimberley Process baada ya kuhakikisha kuwa mapato yake hayatumiwa kuchochea migogoro.


'Uamuzi wa ushindi'


Katika taarifa yao WDC linasema upenyo huo umetoa fursa ya kuuuza nje mara moja almasi isiyosafishwa kutoka kwa kampuni mbili za machimbo ya almasi za Marange Resources na Mbada.

Serikali ya Zimbabwe inamiliki Raslimali zote za Marange na ina asilimia 50 kwenye mgodi wa Mbada, ambayo ina ubia na wawekeza jiwa Afrika Kusini, Reuters linaripoti.

Makampuni mengine ni Anjin Zimbabwe, na ubia wa 50-50 kati ya serikali za Zimababwe na China yataanza kuuza almasi baada ya ujumbe wa Kimberley Process uliozuru machimbo hayo wiki mbili zijazo, linaripoti.

Rais wa WDC Eli Izhakoff ameelezea makubaliano hayo kuwa ni hatua muhimu.

"Inaonyesha kimsingi kuwa Kimberley Process inatoa mwongozo ambao maadili yake kuhusu mkondo wa almasi ambayo haijasafishwa unaweza kulindwa wakati huo huo unatengeneza faida ya mapato yake kutokana na raslimali," alisema.

Bw Izhakoff alisema Muungano wa Ulaya umeshiriki kikamilifu kumaliza kizuizi hicho.

"Sifa pia ziende kwa Zimbabwe, mataifa ya Afrika yakiongozwa na Afrika Kusini na watu binafsi ambao walitumia mudfa mrefu wa mipango na majadiliano," alisema.

Mwezi Juni serikali ya DRC – baada ya kuwa mwenyeji wa kundi la Kimberley Process ilitoa taarifa rasmi ikisema imefikia makubaliano ya kuodnoa marufuku hiyo.