Na MWANDISHI WETU
Kitanda usichokilalia kamwe huwezi kujua kunguni wake ni wapole au wakali kiasi gani! Tangu ndoa ya kifahari ya Irene Pancras Uwoya na Hamad Ndikuma ‘Kataut’ iingie kwenye gogoro zito Novemba, 2011, bado hali si shwari, Ijumaa lina kitu kamili.

Mbali na gogoro hilo la kindoa, pia kuna ishu ya madai ya Ndikumana kumtorosha mtoto wao kwa siku kadhaa na baadaye kumrejesha bila maelezo ya alikompeleka.

NYUMA YA PAZIA KUNA SIRI NZITO
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa wanandoa hao, nyuma ya matukio yote hayo, kuna siri nzito na ukweli ni kwamba mambo hayo yalianza siku nyingi.

VIASHIRIA VYA DAKIKA ZA MWISHO WA NDOA YAO
Ilidaiwa kuwa, pamoja na jitihada kubwa zilizofanywa na magazeti ya Global Publishers, kurejesha uhai wa ndoa hiyo iliyotaka kuota mbawa, kumekuwa na matukio mengine yanayoashiria mwisho mbaya wa muunganiko wao.
MTOTO KUACHWA KWA BIBI YAKE
Kwa mujibu wa Uwoya, yeye na mumewe wameshahama kwa mama yake Mbezi Jogoo, Dar es Salaam na kumuacha mtoto akiwa na miezi sita na siku kadhaa na kwenda kupanga Sinza-Madukani, Dar huku jukumu la kumlea mtoto likibaki kwa bibi mtu na ‘hausigeli’.

ETI UWOYA YUKO ‘LOKESHENI’ MUDA WOTE!
Hata hivyo, suala hilo liliibua maswali yaliyokosa majibu ambapo katika hali ya kushangaza, mtoto huyo alipokuwa anaumwa, Uwoya alimwachia majukumu mumewe kwa madai kwamba yeye yuko kambini au ‘lokesheni’ muda wote kwa ajili ya filamu (haikutajwa jina).



DALILI MBAYA ZAONEKANA KWENYE ‘BETHIDEI’ YA UWOYA
Desemba 18, 2011, ilikuwa ‘bethidei’ ya Uwoya iliyofanyika kwenye bustani iliyopo Tangi Bovu, Mbezi Beach, Dar ambapo katika hali ya kushangaza, Ndikumana hakuwa na furaha hata kidogo.

Kwa mujibu wa ‘shujaa’ wetu aliyekuwa ndani ya pati hiyo, kuliibuka minong’ono mingi pale Uwoya alipomlisha keki mumewe kama vile hamjui huku akiwakumbatia kwa bashasha mastaa wa kiume Bongo (kuna ushahidi wa picha).
ETI KUNA MANENO YALIMUUDHI UWOYA
Hata hivyo, kwa mujibu wa Uwoya, kuna maneno yaliyosemwa na Ndikumana mahali hapo ambayo hayakumfurahisha.
Utamaduni wa kawaida unaweka wazi kuwa wanandoa wanapotofautiana mbele za watu (mbaya zaidi kwenye pati), hawapaswi kuonesha kwa wageni hadi wanapokuwa wawili ndipo huwekana sawa.
HAWAKUSHEREHEKEA KRISMASI PAMOJA
Ishara nyingine mbaya hasa katika msimu wa sikukuu ambapo watu hujumuika na familia zao, katika sherehe ya Krismasi, wanandoa hao inadaiwa hawakusherekea pamoja.

KWA NINI?
Uchunguzi wa Ijumaa unaonesha kuwa, ndicho kipindi ambacho Ndikumana ambaye ni mwanasoka wa Rwanda alipopotelea kusikojulikana na mtoto.

UWOYA ACHANGANYIKIWA
Pamoja na kuchanganyikiwa akihaha kumpata mwanaye wakati wa Krismasi, lakini kuna maelezo kuwa Uwoya asingeweza kujumuika na familia yake kwani pia alikuwa ‘bize’ na mambo ya ‘lokesheni’.

UWOYA LAIVU
Ijumaa lilipotaka kujua kuna siri gani nyuma ya mambo hayo yote, Uwoya alisema:
“Mimi simuelewi Ndikumana kwa sababu kulikuwa na ugomvi wa kawaida tu. Zaidi mimi sijui chochote.”
NDIKUMANA AOMBA ASISEME CHOCHOTE
Ijumaa lilifanya jitihada za hali ya juu kumpata Ndikumana ambaye amekuwa hapatikani kirahisi, lakini alipopatikana juzi kupitia kilongalonga cha kiganjani na kusomewa mkasa ‘eituzedi’ alisema kwa kifupi:
“Jamani, please (tafadhali), naomba nisiseme chochote.”

TAHADHARI KABLA YA HATARI
Ukisoma maelezo haya mstari kwa mstari, utabaini kuwa kuna siri nzito iliyojificha baina ya wanandoa hao.
                                                   
CHANZO CHA HABARI NI HAPA.