KUNDI la muziki wa mwambao la Jahazi Modern Taarab chini ya Mkurugenzi wake, Mzee Yusuf ‘Mfalme’ (videoni juu) linatarajia kuzindua albamu yake ya Mpenzi Chokolate Desemba 24, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar.
Akizungumza na Ijumaa, Mzee amesema kuwa, mbali na uzinduzi wa albamu hiyo, siku hiyo kundi lake litasherehekea miaka sita tangu kuanzishwa kwake.
“Itakuwa siku maalum kwani hata Naad Ikwaan Swafaa (kundi linalopiga muziki wa taraab asilia la Zanzibar) litakuwepo kupamba uzinduzi huo sambamba na msanii wa Bongo Fleva, 20% (Hamis Kinzasa),” alisema Mzee.

Ndani ya albamu hiyo Mzee ameimba wimbo uliobeba jina wa ‘Mpenzi Chokolate’, nyimbo nyingine na waimbaji wake wakiwa kwenye mabano ni ‘Sina Muda huo’ (Leila Rashid), ‘Zibeni Njia’ (Khadija Yusuf) na ‘Full Shangwe’ (Prince Amigo).