Sudan Kusini imeishutumu Sudan kwa kufanya mashambulio zaidi katika ardhi yake na dhidi ya majeshi yake.
Gavana wa jimbo la Unity amesema watu kadha wameuawa katika mji mkuu wa jimbo hilo Bentiu wakati ndege ilipodondosha mabomu katika soko moja.
Sudan Kusini pia imesema vikosi vyake vilishambuliwa na ndege katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Heglig ambalo lilitekwa na majeshi ya Sudan Kusini.
Balozi wa Sudan nchini Uingereza, Abdullahi Al Azreg, amesema Sudan haikuwalenga raia.
Amesisitiza kuwa Sudan, Kahrtoum ilipiga kambi za kijeshi zilizotumiwa na waasi wa kaskazini ambao wanasaidiwa na Sudan Kusini.
Mapema Jumamosi Sudan Kusini ilisema kuwa iliyarudisha nyuma majeshi ya adui kutoka maeneo yao karibu na Heglig.
Makamu wa Rais Riek Machar amesema mapigano ya ardhini yalifanyika Ijumaa, kilomita 30 kaskazini mwa Heglig.
Sudan Kusini ilitwaa kisima cha mafut cha Heglig, Jumane iliyopita, na kuchochea shutuma kimataifa na hofu ya kuzuka vita kamili kati yake na majirani zao wa kaskazini.
Sudan Kuini iliingia katika kisima cha mafuta cha Heglig ikiwa ni kujibu kile ilichokiita mashambulio kutoka kaskazini mwa mpaka.

Viongozi wa Sudan, Khartoum wamechukizwa a kitendo cha jirani zao kusini kunyakua kisima cha mafuta cha Heglig, ambacho kinatambuliwa kimataifa kuwa ndani ya ardhi ya Sudan, Kahrtoum.
Muungano wa Afrika umeitaka Sudan Kusini kuondoka katika neo hilo bila masharti yoyote.
Jeshi la Sudan lilithibitisha Ijumaa kuwa lilifaya mashambulio ili kulirejesha eneo la Heglig katika himaya yake baada baada ya serikali ya Khartoum kuapa kutumia kila njia katika kukabiliana na uchokozi wa majeshi ya Sudan Kusini.
Naye msemaji wa jeshi la Sudan kanali Sawarmi Khalid alisema Jumamosi kuwa eneo la Heglig lilikuwa tayari kwa asilimia mia moja chini ya udhibiti wao.