Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Magese Mulongo (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, jana tayari kwa  kuhudhuria Mkutano wa  45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika utakaoanza tarehe 20 hadi 27 Julai Mjini Arusha ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa kongamano hilo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka

 Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka alipokwenda kukaguwa Ukumbi wa Ngurudoto, Arusha , jana, patakapofanyika Mkutano wa  45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa kongamano hilo. 
Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akitowa maelekezo kwa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa  45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika alipotembelea Ukumbi wa Ngurudoto, mkoani Arusha  patakapofanyika kongamano hilo ambapo Tanzania ndio mwenyeji