Stori: Hamida Hassan, Gladness Mallya na Musa Mateja.
Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha (jina tunalihifadhi kwa sasa) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la kifahari.


Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na begi la fedha.
TWENDENI USHUANI
Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake.

Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze ‘vizuri’ na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ‘kamwendo’.
Nje ya nyumba hiyo kuna ‘parking’ ya magari madogo zaidi ya kumi huku chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua ya kuvutia.“Amehamia hivi karibuni, anaonekana muda wa kutoka na kuingia tu.