"Mjini Moshi kunafukuta moto 2015" 

                  CCM WAVUNA WANACHAMA 24 KUTOKA CHADEMA

 Mkutano wa CCM mjini Moshi, Jumamosi 18 April 2015

Wanachama wa CCM na viongozi wao mjini Moshi walifanya mkutano wa hadhara katika maeneo ya Pasua,Moshi mjini siku ya jumamosi 18 April 2015,
katika mkutano huo ulioudhuriwa na mamia ya watu uliweza kuvuta hisia za wengi na katika waliovutika ni pamoja na wanachama 24 wa CHADEMA ambao walirudisha kadi za Chadema na kujiunga na CCM.
Jimbo la mjini Moshi limekuwa gumozo la kiasa kabla ya uchaguzi mkuu kutoaka na baadhi ya wananchi na vikundi mbali mbali vya kijamii kujitokeza kwa kumshawishi kijana moja ajulikanae kwa jina la Daudi Babu Mrindoko achukue fomu za kugombea ubunge 2015,kitendo hiko cha kumshawishi kijana huyo ,kimekuwa kama cheche za moto zilinazosemekena kuwa baadhi ya vigogo kujitangaza kutogombe tena nafasi zao za udiwani na ubunge.
Baadhi ya wakazi wa Moshi wanadai kuwa wanataka mabadiriko 2015 wapate mbunge kijana mwenye uwezo na wepesi wa kuwatumikia,ambaye atakuwa kiungo wa jamii yote ya wakazi wa Moshi,wanajaribu kushawishi kijana Daudi Mrindoko lakini mwenyewe bado yupo kimya ! wenyewe wanamwita Obama wa Moshi mjini.