Saud Arabia imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Iran na huku kukiwa na hali mbaya ya mvutano kufuatia utekelezaji adhabu ya kifo kwa mhubiri maarufu wa dini ya kiislamu kutoka mjini Riyadh .
Waziri wa mambo ya kigeni wa Saud, Adel al-Jubeir, ameishutumu serikali ya Iran kwa kusambaza silaha na kuanzisha jela na kuwafunga watu wanaodhaniwa magaidi katika ukanda wake .

Waziri huyo ameongeza kusema kwamba ,wana diplomasia wa Iran wametakiwa kuondoka Saudia ndani ya saa arobaini.Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandamanaji mjini Tehran waliuvamia ubalozi wa Saudi ,huku wakilaani utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa Sheikh NIMR al-NIMR na watu wengine arobaini na sita.
Watu hao waliouawa inasadikiwa walikuwa na hatia ya makosa yanayohusiana na ugaidi.kiongozi mkuu wa Iran alimuelezea Sheikh huyo kama shahidi ambaye alikuwa akitetea amani na kufanya maandamano ya amani.