Rais wa Brazil, Dilma Rousseff amehaidi kupambana mpaka mwisho na jitihada zinazompinga ili kutetea demokrasia ya Brazil.Mwishoni mwa juma lililopita baraza la seneti liliweza kuhalalisha tuhuma hizo kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais Rousseff ambaye ameshutumiwa kwa kufanya mabadiliko katika bajeti ya fedha jambo ambalo lilishutumiwa vikali.
Katika hatua yake ya kwanza ambayo raisi huyo kufanya baada ya kura kupigwa ,amesema dhamira yake ilikua safi na hajafanya jambo lolote kinyume cha sheria.
Baraza la seneti linatarajia kufungua mashitaka ya mtu kupigiwa kura ya kutiliwa shaka ifikapo mwezi ujao na kumfanya rais kusimamishwa katika wadhifa wake kwa muda wakati kesi ikiendelea.
Lakini Rais Rousseff alisema hana mpango wa kuachia wadhifa wake huo na kusema "nitaendeleza mapambano haya kwa kupitia taratibu zote,kuanzia hiyo iliyowekwa na baraza la seneti kwa kuwa nina uhakika nitaweza kupata fursa ya kujitetea."
|
0 Comments