Akiweka kimiyani goli 5 pekee yake kati ya goli saba walizofunga Manchester United dhidi ya Blackburn Rovers na kuendelea kuin'gan'ganiza Manchester united katika nafasi ya tatu ndani ya msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.Ligi hiyo haikuwa tu Old Trafford bali viwanja vingine viliwaka moto pia,Wakati Arsenal anamuaibisha nyumbani kwake Aston Villa kwa goli 4-2,Huku vijana wa Westham united wakiibanjua Wigan Athletic kwa goli 3-1 na wakali Wolverhampton Wanderers wakipeta uwanja wao wa nyumbani kwa kuifunga goli 3-1 timu ya Sunderland.Dozi haikuishia hapo kwani West Bromwich nayo ilibamiza bila huruma Evaton kwa goli 4-1,timu zilizokwenda sare ni Stroke City ambao walishindwa kuonyeshana ubabe na Manchester City kwa sare ya 1-1,Fulham ililazimishwa sare pia ya goli 1-1 na Birmigham City.
Kesho ligi hiyo itaendelea kwa timu kubwa kuonyeshana ubabe.Usikose kuangalia Maganga One Blog kwani tutakuletea kila habari juu ya ligi hii hapo kesho.