Ni kawaida kwa raisi Obama kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu pindi akiwa hayupo bize na shughuli za kikazi.Kabla hajakuwa na majukumu mengi ya kikazi haikuwa jambo geni kumuona Barack Obama akikimbizana uwanjani kukiputa kikapu(basketball).Jana ijumaa raisi Barack Obama kama kawaida yake na wasaidizi wake uwanjani wakicheza  mpira  Ray Decerega kwa bahati mbaya alimgonga mdomoni raisi Obama na kiwiko(kipepsi) na kumsababishia majeraha maubwa ya mdomo kuchanika.Raisi Obama alipata matibabu ya awali kabla ya kupelekwa hospital kwa matibabu zaidi.raisi Obama kashonwa nyuzi 12 kwenye  mdomo ambako alichanika.Hali ya raisi inaendelea vizuri.Maganga One Blog inampa pole raisi Barack Obama.