Polisi wa Marekani na Mexico wamegundua njia nyingine ya siri chini ya ardhi mpakani inayotumiwa na makundi ya wauzaji dawa za kulevya.
Maafisa wa usalama wamesema njia hiyo inaunganisha nyumba moja iliyopo mjini Tijuana nchini Mexico na bohari iliyopo Otay Mesa, katika jimbo la California nchini Marekani.
Njia hiyo ina mfumo wa reli, taa za kisasa na mfumo wa kuweka hewa baridi na iko karibu sana na njia nyingine kama hiyo iliyogunduliwa wiki tatu zilizopita.