Wanajeshi wa Brazil wenye silaha nzito, wameuteka mtaa wa maskini wa Rio de Janeiro wenye fujo nyingi, ambako mamia ya wauza mihadarati walikuwa wamezingirwa kwa siku kadha.
Wanajeshi na polisi zaidi ya elfu mbili walianza shambulio lao alfajiri, katika mtaa wa Alemao mjini Rio, wakisaidiwa na helikopta na magari ya deraya.Mapambano makali ya risasi yalisikika. Mwandishi wa BBC mjini Rio, alisema kazi inaendelea hivi sasa, ambapo askari wa usalama, wanafanya msako katika kila nyumba kuwatafuta wauza dawa za kulevya.
Tangu msako kuanza siku chache zilizopita, watu wapatao 45 wameuwawa na magari yanayofikia mia yameangamizwa.
0 Comments